WAZIRI
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola ametoa wiki mbili kwa Jeshi
Polisi Mkoa wa Kigoma, kuhakikisha linakomesha matukio ya ujambazi
yaliyokithiri katika Wilaya ya Kibondo pamoja na sehemu zingine mkoani
humo.
Lugola
aliongeza kua, katika kupambana na majambazi hao ambao wanasumbua
wananchi wilaya hiyo ya Kibondo na kukosa amani katika maeneo yao,
polisi ifanye operesheni maalumu kuwatia mbaroni watuhumiwa hao.
Akizungumza
na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa
Community Centre mjini Kibondo, leo, Lugola alisema katika operesheni
hiyo pia itambatana na utoaji onyo kwa watu wasio waaminifu
wanaowahifadhi raia wa kigeni ambao wengi wao ni wahalifu.
‘’Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kigoma, natoa wiki mbili tu, kwa kushirikiana na Mkuu
wa Wilaya fanyeni operesheni ya kuwasaka majambazi hawa usiku na mchana
mpaka jambazi wa mwisho awe amekamatwa,’’ alisema Lugola.
Lugola
alisema haiwezekani tukasalimu amri kwa majambazi, haiwezekani
kunyoosha mikono kwa jambazi waliopo katika maeneo mbalimbali wa wilaya
hiyo pamoja na mkoa kwa ujumla.
Waziri
Lugola pia aliwataka wananchi wilayani humo kutoa taarifa polisi za
wahalifu hao ili kuwezesha operesheni hiyo ifanikiwe zaidi na wananchi
waweze kuishi kwa amani na kufanya shughuli zao za kuijenga nchi.
Waziri
huyo pia licha ya kusema anajua changamoto mbalimbali zinazowakibili
polisi ikwemo ukosefu wa magari lakini aliwataka aliwataka wawahi
katika matukio ya uhalifu yanapotokea, wanaweza kutumia pikipiki ili
kuwahi kwa wakati katika matukio hayo.
Waziri
Lugola yupo katika ziara ya kikazi Mkoa wa Kigoma ambapo anatembelea
Wilaya zote mkoani humo kwa kufanya kikao na watumishi walio chini ya
wizara yake pamoja na kuzungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara
kwa ajili ya kusikiliza kero zao pamoja na kuzitatua.
Mpekuzi.
Comments