Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema suala la mtuhumiwa
kukaa mahabusu saa 24 linazingatia suala la upelelezi wa awali hivyo mtu
akitolewa humo kusaidia kupeleleza muda huanza kuhesabiwa upya
anaporudishwa ndani.
Amesema,
kwenye Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai mtuhumiwa anapokamatwa kwa
mara ya kwanza na kuwekwa mahabusu anaweza kutolewa kabla ya kufika saa
24 kwa ajili ya upelelezi au kwenda kuonesha silaha au kuonesha
ushahidi kutokana na maelezo yake.
"Mnapomtoa
atakaporudi mahabusu huyo mtuhumiwa anaanza kuhesabiwa masaa yake upya.
Sasa kwa bahati mbaya wananchi wanahesabu tangu tangu alipokamatwa
lakini kisheria tunahesabu tofauti"alisema jana Waziri Lugola wakati
anajibu swali la Mbunge wa Tarime Vijijini John Heche.
Heche
alitaka Waziri Lugola atoe tamko kwamba polisi wazingatie sheria na
iwezo marufuku kwa mtuhumiwa kuwekwa mahabusu zaidi ya saa 24 bila
kufikishwa mahakamani.
Lugola alisema, si nia ya Serikali kutesa wananchi hivyo askari watakaokiuka sheria hiyo ya mahabusu saa 24 watachukuliwa hatua.
"Hakuna
yeyote ambaye sisi tunamfumbia macho. Kwa hiyo Mheshimiwa Heche uwe na
amani. Huyo mtu unayemsema huyo tumeshatoa maelekezo, na tunajua concern
yako"alisema Lugola.
Alikiri
kuwepo kwa malalamiko ya wananchi kuwekwa nani na baadhi ya polisi
wasio waaminifu na waadilifu kwa makosa yasiyostahili.
Mpekuzi.
Comments