Hayo
yamesemwa na Afisa mdhamini wizara ya Fedha nd. Ibrahim Saleh Juma wakati
alipokuwa akizungumza na wafanyabiasha wa mkoa wa kusini Pemba katika semina ya
sikumoja juu ya marekebisho ya Sheria kwa mlipa kodi huko katika ukumbi wa
baraza la mji chake chake.
Amesema
kumekuwepo na baadhi ya wafanyabiasha ambao hutoa taarifa za uongo jambo ambalo
linaleta usumbufu mkubwa wakati wa ulipaji wa kodi.
Amefahamisha
kuwa nivyema kwa wafanyabiashara hao kuwa waaminifu pindi wanapo wasilisha
vielelezo vyao kwa bodi ya mapato Zanzibar ZRB ili kurahisisha upatikanaji wa
taarifa zao kiukamilifu.
Aidha
amewakumbusha wafanyabiashara hao kuwa na utaratibu wa kujiwekea kumbu kumbu
ili ziwarahisishie wao na wakaguzi wanapofika kutafuta takwimu hizo.
Akiwasilisha
mada ya mabadiliko ya sharia zilizo fanyiwa marekebisho Mwanasheria wa Bodi ya
mapato Zanzibar ( ZRB ) Khamis Jafar Mfaume amewataka wafanya biashara hao
kuzielewa vyema sharia hizo ili kuepuka malamiko yasio yalazima wakati wa
ulipaji wa kodi.
Amesema
kuwa lengo la kurekebishwa kwa sharia hizo nikuondoa changamoto zinazojitokea
kwa walipa kodi ili ziweze kutekelezwa kwa muda muafaka na bila pingamizi.
Akizitaja
sharia zilizo fanyiwa marekebisho kuwa ni pamoja na Sheria ya Usimamizi wa
kodi, Sheria ya ushuru wa Stamp, Sheria ya kodi za mafuta na Sheria ya rufaa ya
Kodi.
Kwaupande
wao wafanya biasharao hao wameitaka Serekali ya mapinduzi Zanzibar kupitia Bodi
ya mapato ZRB kuwasimamia kikamilifu
wafanya biashara wote wanokwepa ulipaji wa Kodi ili kuweza kuleta maendeleo
nchini.
Comments