Dkt Tizeba Asema Bei Ya Korosho Imeimarika Kutokana Na Matumizi Bora Ya Mfumo Wa Stakabadhi Ghalani Na Ushirika.
Uwepo
wa mfumo wa stakabadhi ghalani umekuwa ni mkombozi pekee kwa wakulima
wadogo na wa kati kwa kuwawezesha kupata bei nzuri ya mazao yao,
ukilinganisha na bei zilizokuwa zinatolewa na wafanyabiashara
wanaponunua mazao yakiwa shambani kwa kutumia vipimo ambavyo sio sahihi.
Kabla
ya mfumo huo kuanza wakulima walikuwa wakipunjwa bei ya mazao na
wafanyabiashara ambapo hata hivyo kumekuwepo na mwamko miongoni mwa
wakulima, kupitia vyama vyao vya msingi, wa kutumia mfumo halisi wa
stakabadhi ghalani pasipo kuchukua mikopo toka Taasisi za Fedha. Katika
msimu wa mwaka 2017/2018 vyama vyote viliweza kukusanya na kuuza mazao
bila kukopa benki.
Hayo
yamebainishwa tarehe 29 Septemba 2018 na Waziri wa Kilimo Mhe Mhandisi
Dkt Charles Tizeba (Mb) wakati akifungua Mkutano Mkuu wa wadau wa tasnia
ya korosho uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Benki kuu ya
Tanzania tawi la Mtwara.
Alitaja
kuwa ushirika ni dhana ya kuleta maendeleo kwa kushirikiana, Dhana hiyo
imefanikiwa kuleta mabadiliko ya kiuchumi na kijamii katika kipindi cha
miaka kadhaa iliyopita ambapo uanzishwaji wa vyama vingi vya ushirika
kwa sasa unatokana na elimu watu wengi waliyoipata kuhusu Ushirika.
“Ni
wazi kuwa katika kipindi cha miaka miwili hivi, imani kwa vyama vya
ushirika imeongezeka na vyama vingi vinaendelea kuundwa hasa vile vya
kuweka na kukopa, yaani SACCOS” Alikaririwa Dkt Tizeba
Dkt
Tizeba alitoa wito kwa vyama vya ushirika kuendelee kukusanya korosho
kwa msimu huu ili soko na bei iendelee kuwa imara pamoja na kuwa na
misuko suko mingi ya masoko Duniani.
“Aidha
ni vyema Wakulima wote wakajiandisha na kuwa Wanachama wa vyama vya
Ushirika amabpo watapata faida nyingi ikiwemo kufanya maamuzi kwa
pamoja” Alisema Dkt Tizeba
Alitaja
mafanikio katika zao hilo kuwa ni pamoja na kuimarishwa kwa usimamizi
wa zao, uratibu mzuri wa ununuzi na usambazaji wa pembejeo za ruzuku,
usimamizi wa karibu unaofanywa na viongozi wa serikali katika ngazi
zote, na hamasa mpya ya wakulima kujishughulisha na kilimo cha korosho
katika maeneo asilia na maeneo mapya.
Dkt
Tizeba alisisitiza kuwa hali hiyo ikiendelea kuna uwezekano wa
kuzalisha zaidi ya kiwango cha sasa na kuwa na malighafi inayoweza
kutumika kwa mwaka mzima kwa kuuza nje na viwanda vya ndani.
Katika
hatua nyingine aliongeza kuwa pamoja na kuwa na mafanikio makubwa
kwenye zao la korosho lakini zipo changamoto mbalimbali ambazo ni pamoja
na kuwepo kwa mashamba makubwa ya mikorosho iliyotelekezwa,
Uchelewashaji wa malipo kwa Mkulima, Wanunuzi kulalamikia upotevu wa
Korosho, ubora hafifu na ubadhilifu, pamoja na Ucheleweshaji wa malipo
toka wa Mabenki kwenda vyama na uwepo wasuspence account ambazo
zinaathiri malipo kwa Mkulima.
Hivyo
katika kufanikisha na kuwa na maendeleo katika zao hilo yanatakiwa
kufanyika mabadiliko ambayo yatahitaji ushirikiano wa wadau na hasa
Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi katika usimamizi ili
kuhakikisha Mkulima anapata fedha kwa Wakati.
Ameelekeza
kuwa katika msimu huu kila Halmashauri ianzishe sehemu maalumu ya
Malipo kwa Wakulima (Payment centre) ambapo wataalamu watasaidia vyama
hususani toka Vyama Msingi kwenda kwa Wakulima baada ya ukokotoaji wa
gharama mbalimbali na kupeleka benki kwa wakati jambo ambalo litasaidia
kubaini mapungufu ya kimalipo kwa mabenki na au unaosababishwa na
Watendaji wa Vyama.
Waziri
Tizeba pia ameelekeza kuwa, Mtiririko wa Malipo kwa Mkulima unapaswa
kusimamiwa vizuri na kila Halmashauri ya Wilaya iwe na kituo
kitakachorahisisha malipo kwa Mkulima mara baada ya fedha kutoka Chama
Kikuu cha Ushirika kwenda AMCOS (Payment Clinc Centre), Secretatiati za
Mikoa, Halmashauri, Kamati za Ulinza, Bodi ya Korosho, Mrajis wa Vyama
vya Ushirika na mabenki kushirikiana kuhakikisha jambo hilo
linatekelezeka ili kumpunguzia Mkulima adha ya Malipo
Mpekuzi.
Comments