Staa wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz amezua gumzo siku ya jana Kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuimba kipande cha wimbo chenye maneno “Zari hodari wa Mapenzi”.
Diamond
ambaye alikuwa Kwenye Mahusiano na Zari kwa takribani miaka minne mpaka
walivyimwagana mapema mwaka huu ameibuka na kusifia ujuzi wa mapenzi wa
mama watoto wake huyo.
Diamond
amesema maneno yake Kupitia kipande cha video Kilichomuonyesha akiimba
wimbo mpya wa Msanii kutoka WCB Mbosso uitwao ‘Hodari’ ambapo ndani yake
amemtaja Zari kama Hodari wa mapenzi.
Comments