Kamati
Kuu Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imempitisha Ramadhani
Hamza Chande kuwa mgombea wa uwakilishi wa Jang’ombe katika uchaguzi
mdogo utakaofanyika Oktoba 12.
Taarifa
iliyotolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole
imesema kamati hiyo chini ya Mwenyekiti Rais John Magufuli iliketi
katika ofisi ndogo za chama hicho Lumumba jijini Dar es Salaam.
Katika
taarifa hiyo, alisema CCM imerudia kuwaonya wanachama wake wanaokiuka
Katiba na kanuni za uchaguzi kwa kuanza kufanya kampeni za chinichini za
urais wa Zanzibar.
“CCM
imetoa karipio la mwisho kwa wana CCM wanaokiuka Katiba, kanuni za
uchaguzi, kanuni za uongozi na maadili kwa kuanza kufanya kampeni za
kificho na za wazi za urais wa Zanzibar na kwenda kinyume na utamaduni
na desturi njema za chama chetu ambazo kwa pamoja hutuongoza kuwapata
viongozi wa CCM na Serikali zake,” imesema taarifa hiyo.
Mpekuzi.
Comments