Mkazi
wa Chanika jijini Dar es salaam, Dotusi Isaya anadaiwa kuwaua watoto
wake wawili, kumjeruhi kwa panga mkewe pamoja na mama mkwe, kisha kujiua
baada ya kukataliwa kuwachukua wanae.
Akizungumzia
tukio hilo, kamanda wa polisi Mkoa wa Lindi, Pudensiana Protas amesema
Isaya alifanya mauaji hayo usiku wa kuamkia jana huko Nachingwea mkoani
humo ambapo mtuhumiwa alikwenda Nachingwea anakoishi mkewe Mariam Lucas
na kujificha pembeni mwa nyumba ambayo haijamaliza kujengwa (pagala)
akimvizia kisha kumkata panga eneo la kisogo na begani.
“Baada
ya kumkata mkewe aliingia ndani ya nyumba (katika) chumba wanacholala
watoto na kukuta wanawe wawili wamelala na watoto wengine, lakini yeye
aliwaua wanawe kwa kuwakatakata”, amesema Kamanda.
Kamanda
amesema kuwa Isaya ameamua kufanya tukio hilo baada ya mkewe kumkatalia
asiende na watoto wake Bukoba baada ya kuondoka jijini Dar es salaam
walikokuwa wakiishi awali, ambapo mke wake alimwambia mume wake kuwa
watoto wakiwa wakubwa atawachukua, lakini kwa sasa ataendelea kuishi nao
kwa kuwa bado ni wadogo.
Kamanda
ameongeza kuwa kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, wamesema walianza
kusikia vilio saa sita usiku na walipofika eneo la tukio waliwakuta
majeruhi wawili (Amanda na Mariam) pamoja na maiti za watoto wawili
pamoja na mtuhumiwa akiwa amejinyonga.
Hilo
si tukio la kwanza la mzazi kuua watoto wake kwani Aprili 2017, mkazi
wa Bukoba, Respicius Deogratius aliwaua wanaye mapacha waitwao Nyakato
na Nyangoma kwa kuwakata vichwa.
Tukio
jingine ni la Aprili mwaka huu ambapo Pius Salum, mkazi wa Matai,
Kalambo mkoani Rukwa alimuua mtoto wake, Benedicto Salum (13) kwa
kumpiga ngumi na mateke tumboni akidai si wake.
mPEKUZI.
Comments