Afisa mdhamini wizara ya maji, ardhi nyumba na nishati atoa neno kwa wananchi wa Mfikiwa Chake chake Pemba.


Image result for Juma Bakar AlawiAfisa mdhamini  wizara ya maji, ardhi  nyumba  na nishati Juma Bakar Alawi amewataka wamiliki wa mali zilizo karibu na barabara kuruhusu kufanyika kwa harakati za kimaendeleo  katika barabara hizo.

Amesema hakuna sababu kuona baadhi ya watu wanakwamisha  harakati hizo ikiwemo ujenzi wa barabara na mambo mengine  na kusababisha mivutanao isiyo na ulazima.

Ameyasema hayo  huko katika shamba la mivinje  Mfikiwa Chake chake linalomilikiwa na Nassor Moh’d Issa  katika kulifanyia tathmini ya thamani ya mali zilizomo ili kupisha ujenzi wa barabara kwenye eneo la Polisi Mfikiwa. 

Afisa mdhamini huyo amesema mizozo katika kuleta maendelo haileti tija hivyo ni budi kwa wamiliki wa rasilimali na taasisi kukubaliana na kuondoa tofauti zao ili kazi iendelee kama ilivyopangwa.

Katika hatua hiyo Sheha wa Shehia ya Mfikiwa Bimkubwa Rajab Tangwi amesema chanzo cha mzozo huo kilitokana na mmiliki wa shamba hilo kukataa kukubaliana na tathmini ya awali ya shilingi milioni tisa huku mwenyewe akihitaji milioni 35.

Naye mwakilishi wa mmiliki mwenye shamba hilo la Mivinje Said Moh’d Issa amesema ameridhishwa na tathmini ya sasa lakini kauli sahihi iko kwa mwenye mali ambaye yuko Tanzania bara.

Shamba hilo la mivinje liko kwenye kona mbaya na  meneja wa ujenzi wa barabara hiyo Amini Khalid Abdalla amesema lazima waondoe sehemu ya miti hiyo  ili barabara iweze kuwa bora na kiwango kinachokubalika kwa usalama wa watumiaji wa barabara hiyo .

Comments