Waziri Lugola Atoa Onyo Kali Kwa Makampuni Binafsi Ya Ulinzi, Asema Yanaajiri Vikongwe, Atoa Mwezi Mmoja Kujirekebisha.
WAZIRI
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, ametoa mwezi mmoja kwa
Makapuni binafsi ya Ulinzi kuhakikisha yanarekebisha mfumo wao wa
kuajiri pamoja na utoaji wa mishahara kabla ya Wizara yake haijaanza
kuyahakiki makampuni hayo.
Lugola
amesema baadhi ya Makampuni hayo yameajiri wazee wasiojiweza ambao muda
wote wanalala na wanasabaisha uhalifu kuendelea kwa kasi, wakati vijana
wapo wengi wenye nguvu zao wanaweza wakazifanya kazi hizo kwa umakini
zaidi, na pia tatizo lingine wanalipwa mishahara midogo hali hiyo
inawafanya pia wajiingize katika uhalifu.
Akizungumza
na mamia ya wananchi mjini Bunda, mkoani Mara katika mkutano wa hadhara
uliofanyika Stendi ya zamani mjini hapo, Waziri Lugola alisema,
Serikali ya awamu ya tano kamwe haitataka uzembe, hivyo makampuni hayo
yanayovunja utaratibu huo siku zao zinahesabika.
Lugola
aliongeza kua, licha makampuni hayo yamekua yakiwekeza nchini na pia
yanasaidia kufanya doria katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo ya
miji, lakini yapo maeneo machache baadhi ya makampuni yanavunja sheria
ya nchi kwa kufanya mambo kinyume na sheria inavyowaelekeza.
“La
kwanza kabisa makampuni haya yanafanya mambo ya hovyo kwa kuajiri
vikongwe kufanya kazi za ulinzi, utamkuta kikongwe kavaa sare ukimuuliza
anasema mimi ni mfanyakazi wa kampuni fulani, hii haikubaliki hata
kidogo, kwasababu kwa umri ule hawawezi kupambana na wahaarifu, na kwa
umri ule muda wote usinzia na baadhi yao unyang’anywa silaha,” alisema
Lugola.
Pia
lugola alisema kitendo cha baadhi ya makampuni hayo kulipa mishahara
midogo, au kutowalipa kabisa wafanyakazi hao, hiyo hali inasababisha
uhalifu kwasababu wafanyakazi hao hawataridhika na kipato duni hivyo
uweza wakashirikiana na wahalifu au wenyewe kushiriki matukio hayo.
“Nataka
makampuni haya yajirekebishe na yasipojirekebisha ndani ya mwezi mmoja
ambapo tunataka kuyaakiki makampuni haya, wasije wakamlaumu waziri wa
mambo ya ndani ya nchi ambapo yapo baadhi ya makampuni tutaondoa
tulichoridhia ili wasifanye kazi katika nchi hii,” alisema Lugola.
Aidha,
Lugola aliwataka askari polisi nchini wahakikishe wanafanya kazi kwa
weledi na endapo askari atawaonea wananchi kwa kuwabambikizia kesi,
kuwaomba rushwa, ameapa katika uongozi wake atahakikisha anawaondoa.
Pia
Lugola aliwataka madereva wa magari yakiwemo mabasi pamoja na bodaboda
kua makini kwa kufuata sheria za barabarani kwa kuwa, Rais John Magufuli
wakati anamuapisha aiongoze wizara hiyo, alisema amechoshwa na ajali
zinazotokea nchini ambazo zinamfanya atoe rambirambi kila siku, hivyo
yeye kama Waziri husika, hatakubali kuona madereva wanafanya uzembe
barabarani.
Katika
mkutano huo ulioandaliwa na ofisi ya mkuu wa wilaya, ulihudhuriwa na
viongozi wa wilaya hiyo pamoja na mamia ya wananchi wa Bunda ambapo
baadhi ya wananchi walipewa nafasi ya kumuuliza maswali Waziri huyo.
Hata hivyo, Waziri Lugola aliyajibu maswali hayo ambapo baadhi ya
maswali yalililalamikia Jeshi la Polisi Bunda, baadhi ya askari
wanawanyanyasa wananchi, Lugola aliyajibu maswali yote katika mkutano
huo.
Mpekuzi.
Comments