Chama
cha Wanasheria Tanganyika Law Society, kimelaani vikali kitendo
kilichofanywa na mkuu wa mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti aliyetoa amri
ya kukamatwa kwa mmoja ya wakili wao Menrad De Souza kitu ambacho ni
kinyume cha Sheria ukizingatia hana mamlaka hiyo.
Akizungumza
na Waandishi wa habari jana jijini Dar- esa Salaam Rais wa chama hicho
Bi Fatma Karume alisema juzi mchana mkuu huyo wa mkoa alimkamata
mwanasheria wa chama hicho pamoja na wateja wake waliokwenda ofisini ili
kuingia mkataba baina ya wateja na wakulima ndipo mkuu wa mkoa alipotoa
amri kwa polisi mwanasheria huyo na wateja wake wakamatwe na kuwekwa
ndani kwa masaa 48 kwa amri ya mkuu huyo wa mkoa.
Alisema
chama hicho kimelazimika kutoa taarifa hiyo kwani siyo mara ya kwanza
kwa wakuu wa mikoa na wilaya kutoa amri watu kuwekwa ndani na polisi kwa
masaa 48, hivyo chama hicho kinapinga matumizi mabaya ya madaraka ya
viongozi hao dhidi ya wananchi.
Fatma
alisema hapa nchini hakuna mtu anayetoa hukumu ya mtu kukaa ndani
isipokuwa Mahakama na hiyo ni baada ya kusikiliza pande zote mbili,
hivyo wakuu wa wilaya na mikoa kutoa matamko ya kuwakamata watu ni sawa
na kutoa hukumu jambo ambalo hawapaswi kufanya.
Alitumia
fursa hiyo kueleza utofauti wa kisheria uliopo baina ya Zanzibar na
Tanzania bara kwa kusema kuwa; "Zanzibar huwezi kukaa ndani kwa miezi 9
bila kuhukumiwa hapo utapata dhamana moja kwa moja, hapa bara watu
wanakaa miaka 9 mpaka 10 na hii ndio tofauti ya Sheria za Tanzania Bara
na Zanzibar".
Aliongeza
kuwa ...." Kuna changamoto kubwa sana kwa mawakili wetu kukaa ndani kwa
muda mrefu, tatizo ni Tanzania Bara na sio Visiwani, bunge la huku
Tanzania bara likipitisha Sheria siyo kwamba kesi hii hakuna kupata
dhamana basi ndo imepita hapanaa hii ni sheria ovu".
Kwa
upande wake wakili msomi Jebra Kambole alisema wakili huyo amekamatwa
akiwa anatimiza majukumu yake ya kikazi, na kwamba Wakuu wa mikoa
wamekuwa wakitumia sheria vibaya kuwaumiza wananchi na watu wengine
kinyume na sheria.
"Kuna
sheria na matumizi mabaya ya sheria, kwahiyo Wakuu wa mikoa wamekuwa
wakitumia vibaya sheria na matokeo yake wanawaumiza wananchi, waandishi
wa habari na wengine" aliongeza wakili Kambole.
Mpekuzi.
Comments