Serikali
imesema inaandaa kanuni zitakazoruhusu kufanyika uwindaji wa kiasili
(Local Hunting) kwenye maeneo ya wazi kwa ajili ya kitoweo ili wananchi
waweze kunufaika moja kwa moja na Maliasili zao ili waone umuhimu wa
kuhifadhi.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga amesema hayo jana wakati
alipokuwa akizungumza na Menejimenti ya Hifadhi ya Taifa ya Mikumi
ikiwa ni muendelezo wa ziara zake za kikazi mkoani Morogoro kwa ajili ya
kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili Maliasili, Malikale na
Uendelezaji Utalii.
Amesema
wawindaji hao watapewa vibali maalum vitakavyowawezesha kuwinda kwa
ajili ya kujipatia vitoweo vya nyamapori na kutakuwa na maeneo maalum
kwa ajili ya kuuzia vitoweo hivyo kwa jamii.
Aidha,
Ametaja aina za vitoweo vitakavyokuwa vinauzwa kwenye maeneo hayo
maalum ikiwa pamoja na nyama ya mamba, nyati,swala viboko na wengineo.
Kwa
upande wake, Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi za Taifa za Mikumi, Godwell Ole
Meng'ataki amesema kama kutakuwa na utaratibu mzuri itaweza kusaidia
kuongeza mapato kwa nchi.
Aliongeza
kuwa utaratibu huo wa kuwa na sehemu maalum ya kuuzia vitoweo si mgeni
kwa vile nchi kama Afrika Kusini wamekuwa wakifanya hivyo na pia wana
maeneo maalum kwa ajili ya kuuzia viteweo vya nyamapori.
Mpekuzi.
Comments