Mkuu
wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemas E Mwangela amekataa ombi
la Mkandarasi kutoka kampuni ya Mats Engineering Ltd Paulo Philipo Paulo
la kuongezewa kipindi cha miezi miwili ili aweze kukamilisha ujezi wa
Daraja la Kikamba Wilayani Songwe.
Brigedia
Jenerali Mwangela amekataa ombi hilo jana alipokagua ujenzi wa daraja
la Kikamba linalounganisha kata za Kapalala na Gua wilayani Songwe
kwakuwa sababu alizotoa mkandarasi huyo hazijitosheleji.
Alisema
daraja hilo lazima likamilike kwa muda uliopangwa ambao ni Septemba,
2018 huku mkandarasi huyo akitoa sababu kuwa atachelewa kukamilisha
ujenzi huo kutokana na mvua nyingi zilizonyesha na mwamba mgumu uliopo
eneo la ujenzi.
“Mkandarasi
ahakikishe anafanya kazi mchana na usiku ili akamilishe ndani ya muda
wa mkataba, vifaa vya kumuwezesha kufanya hivyo anavyo na ombi la
kuongezewa muda wa ujenzi mimi siafikiani nalo”, alisema Brigedia
Jenerali Mwangela.
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Songwe Samuel Jeremia alisema yeye na viongozi
wengine wataendelea kusimamia miradi ya maendeleo na katika ujenzi wa
daraja hilo watahakikisha wanamsimamia mkandarasi huyo ili amalize ndani
ya muda uliopangwa.
Daraja
la Kikamba linalolunganisha kata za Kapalala na Gua limeanza kujengwa
mwezi Oktoba 2017 na linatarajiwa kukamilia Septemba 2018 likiwa
limegharimu shilingi bilioni 1.4.
Mpekuzi.
Comments