Kwa kipindi kirefu kumekuwa na stori za hapa na pale kuwa muigizaji wa filamu Bongo, Elizabeth Machael 'Lulu' anaolewa na Majey.
Sasa
basi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda jana August 18,
2018 akiongea na waandishi wa habari alipohudhuria Komaa Concert
aliulizwa kuhusu uwepo wa harusi hiyo.
RC Makonda amesema Harusi ya Lulu na Majey ni miongoni mwa harusi tatu ambazo ni lazima azisimamie.
"Majizo
tayari yupo kwenye mipango na binti yangu Lulu na wameshakuja nyumbani
na wameshafanya vikao vingi vya kupanga kwa ajili ya Harusi," alisema RC
Makonda.
RC Makonda ametaja harusi nyingine mbili ambazo lazima azisimamie ni ile ya Meya wa Kinondoni, na ya Lemutuz.
Mpekuzi.
Mpekuzi.
Comments