Rais
Mstaafu wa awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete jioni ya tarehe 14, Agosti 2018 amemtembelea na kumjulia
hali Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla
aliyelazwa katika wodi maalum kitengo cha Taasisi ya mifupa MOI,
hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Hii
inakuwa ni mara ya pili kwa Kikwete kumtembelea Dk Kigwangalla ambapo
awali alimtembelea Agosti 8, alipokuwa amelazwa Wodi ya Mwaisela
akipatiwa Matibabu ya awali.
Kikwete
amemtakia kila lakheri katika kipindi hiki kwa kuuguza majeraha ya
mkono na sehemu za mwili ikiwemo mbavu ambazo kwa sasa hali yake
inaendelea kuimarika kwa mujibu wa Madaktari wa kitengo hicho cha mifupa
MOI.
Awali
tokea kufanyiwa operesheni ya mkono ameweza kufanya mazoezi taratibu
ikiwemo kutembea mwenyewe katika viunga hivyo vya Muhimbili.
Dkt.
Kigwangalla alipata ajali ya gari mnamo Agosti 4, 2018 huko Manyara
akiwa katika ziara ya kikazi ambapo katika ajali hiyo iliyokuwa na watu
6, watano walijeruhiwa na mmoja alifariki dunia ambaye alikuwa afisa
habari mwandamizi wa Wizara hiyo, Hamza Temba.
Mpekuzi.
Comments