NaneNane Simiyu: Naibu Waziri Wa Kilimo Atao Wito Kwa Wakulima Kutumia Zana Bora Za Kilimo, Kulima Kilimo Chenye Tija.
Naibu
Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt. Mwanjelwa ametoa wito kwa wakulima kote
nchini kulima kilimo chenye tija kwa kutumia zana bora za kilimo ili
kuongeza uzalishaji na kupata mavuno mengi na bora.
Dkt.
Mwanjelwa ameyasema hayo Agosti Mosi, mara baada ya kukagua mabanda ya
maonesho ya Kilimo katika Uwanja wa Nanenane wa Kanda ya Ziwa Mashariki
uliopo Nyakabindi Bariadi, katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa
yanayofanyika Kitaifa Mkoani Simiyu.
Dkt.
Mwanjelwa amesema Serikali kupitia Mfuko wa pembejeo unatoa mkopo wa
pembejeo kwa riba ndogo sana, hivyo akatoa wito kwa wakulima wote nchini
kwenda katika Halmashuri zao na kupata utaratibu wa kuomba mikopo hiyo
ili waweze kupata mikopo itakayowawezesha kununua zana bora za kilimo.
“
Nitoe wito kwa wakulima wote nchini wajitahidi sana kwenda kwenye
kulima kilimo cha kisasa kilimo chenye tija, sisi kama Serikali tuna
mfuko wetu wa pembejeo unaotoa mikopo kwa riba ndogo sana, hivyo
wakulima wanaweza kuomba mikopo hiyo na kwenda kununua pembejeo bora za
Kilimo” alisema Dkt. Mwanjelwa.
Katika
hatua nyingine Dkt. Mwanjelwa amewataka maafisa ugani kuwafuata
wakulima shambani badala ya kukaa ofisini, ili kuwapa elimu ya kilimo
bora na kuwawezesha wakulima kufikia lengo la kulima kilimo chenye
tija.
Naye
Baraka Itemu mkulima wa Mpunga kutoka Geita ametoa wito kwa wakulima
wenzake kote nchini kuachana na matumizi ya jembe la mkono na jembe la
kukokotwa na ng’ombe kwa kuwa ni teknolojia iliyopitwa na wakati na
haina tija katika uzalishaji.
“
Mimi ni mkulima wa mpunga binafsi matrekta yamenisaidia sana maana
naweza kulima eneo kubwa kwa muda mfupi na nikapata mazao mengi, natoa
wito kwa wenzangu wanaotumia majembe ya mkono na ya kukokotwa na ng’ombe
waache waende kwenye makampuni ya matrekta wakakope, ili waweze
kuzalisha mazao kwa wingi” alisema Baraka.
Nao
wauzaji wa zana bora za kilimo waliofika katika maonesho ya Nanenane
Bariadi mkoani Simiyu wamesema wako tayari kushirikiana na wakulima ili
kuhakikisha wanapata zana hizo, huku wakibainisha kuwa wakulima
wasiokuwa na uwezo wa kununua zana hizo kwa fedha taslimu wako tayari
kuwakopesha.
Maonesho ya Nananane mwaka 2018 yanafanyika Kitaifa Mkoani Simiyu, ambapo yameanza leo na yatahitimishwa Agosti 08, 2018.
Mpekuzi.
Comments