Multichoice (Dstv) na Zuku hatarini kunyang'anywa leseni za kurusha matangazo Tanzania kwa kukaidi Agizo la TCRA la kutoonyesha televisheni za ndani.
Mamlaka
ya Mawasiliano nchini (TCRA) inakusudia kusitisha leseni ya kampuni ya
Multichoice Tanzania Limited, wamiliki wa king’amzi cha DSTV na Simbanet
Tanzania Limited inayomiliki Zuku kwa kile kinachoelezwa kuwa ni
kukiuka masharti ya leseni.
Taarifa
iliyowekwa kwenye vyombo vya habari na mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo,
leo Agosti 7 inaeleza kuwa kampuni hizo zimejumuisha katika vifurushi
vyao chaneli za ndani ambazo hazitakiwi kulipiwa.
“Simbanet
Tanzania Limited, Multichoice Tanzania Limited, hairuhusiwi kuonyesha
chaneli za televisheni zenye leseni za kutazamwa bila malipo kupitia
ving’amuzi vyao isipokuwa TBC1 peke yake,” limeeleza tangazo hilo.
Tangazo
hizo linasema TCRA imewahi kuziamuru kampuni hizo kuacha kubeba na
kuonyesha chaneli hizo kwa kuwa ni kinyume na matakwa ya sheria na
leseni walizopewa lakini zimekaidi onyo hilo na kuendelea kuonyesha
chaneli hizo.
Limeongeza
kuwa TCRA inakusudia kusimamisha kabisa leseni zote zilizotolewa na
mamlaka hiyo kwa kampuni hizo kwa sababu zimeshindwa kutekeleza amri
halali na masharti ya leseni zao.
Mpekuzi.
Comments