Mkuu
wa mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga ameiagiza
Idara ya Uhamiaji kuanza msako wa kuwakamata wahamiaji haramu
waliojificha kwenye mashamba na majumbani.
Alitoa
agizo hilo jana Jumatatu Agosti 6, 2018 wakati akiwaapisha wakuu wa
wilaya ya Kasulu na Buhigwe ambapo alisema wahamiaji haramu mkoani humo
wanatakiwa kukamatwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria ili
wahukumiwe kifungo.
Kaitka
hatua nyingine RC Maganga alioomba mahakama kuhakikisha kesi zote za
wahamiaji haramu zinapewa kipaumbele ili kupunguza msongamano wa
mahabusu magerezani, ambao wanakula chakula bila kuzalisha.
Alisema
kuna wahamiaji haramu na wakimbizi waliotoroka kambini wanaishi mitaani
na kwenye nyumba za wananchi kinyume cha sheria, jambo ambalo
halikubaliki.
Mpekuzi.
Comments