Ametangaza uamuzi huo leo katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi ndogo za CCM Lumumba jijini hapa, akiwa sambamba na Katibu Mkuu wa chama hicho tawala, Dk Bashiru Ally.
Kuchauka amesema moja ya sababu iliyomuondoa CUF ni utendaji kazi wa Rais John Magufuli pamoja na mgogoro unaokitafuta CUF.
CUF imekumbwa na mgogoro tangu Profesa Ibrahim Lipumba kurejea katika uongozi mwaka 2016, ikiwa ni mwaka mmoja tangu alipojiuzulu uenyekiti wa chama hicho.
Comments