Waziri
wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola ametoa onyo kwa mfanyabiashara Said
Lugumi baada ya kumpa miezi minne ya kukamilisha makubaliano ya mkataba
kati ya kampuni ya Lugumi na Jeshi la Polisi.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani, jijini
Dar es Salaam jana Jumanne Julai 31, 2018 Waziri Lugola alisema kuwa
mahakama ya kushughulikia kesi za rushwa iliyoanzishwa na Rais
Dkt.Magufuli bado haijapata wateja wakati ni wengi wanaoiba fedha za
serikali.
“Mahakama
ya kushughulikia kesi za rushwa inakosa wateja,na wanaoibia serikali
wapo wengi mtaani,na kutokana hili Saidi Lugumi nimempa miezi minne
kukamilisha makubaliano ya mkataba na akishindwa atakuwa mteja wa
mahakama hiyo” amasema Lugola.
Aidha
Waziri Lugola aliongeza kuwa mkataba unaomhusu mfanyabiahashara Said
Lugumi bado unafanyiwa uchunguzi na taasisi ya kuzuia na kupambana na
rushwa nchini (TAKUKURU) na baada ya uchunguzi hatua sitahiki
zitachukuliwa.
Ikumbukwe
kuwa mfanyabishara huyo aliingia katika msuguano na serikali mwaka
2016, ambapo kamati ya bunge ya hesabu za serikali (PAC) ilibaini
ubadhilifu katika mkataba kati ya kampuni ya Lugumi na Jeshi la Polisi
chini ya Mkuu wa jeshi la polisi wakati huo Ernest Mangu.
Mkataba
huo ulisainiwa kwa ajili ya kufungwa kwa mashine za utambuzi wa
alama za vidole (AFIS) kwenye vituo 108 kwa gharama ya shilingi bilioni
37 ambapo kampuni hiyo ilifunga mashine hizo kwenye vituo 14 tu.
Mpekuzi.
Comments