Rais
mstaafu, Jakaya Kikwete, ametaka teknolojia mpya ya kilimo, ufugaji na
uvuvi inayoonyeshwa wakati wa maonyesho ya wakulima na wafugaji maarufu
kama Nanenane, iwafikie wananchi ili kuwakwamua katika umasikini.
Kauli
hiyo aliitoa juzi baada ya kutembelea vipando na mabanda katika
maonesho hayo Kanda ya Mashariki yanayoendelea katika viwanja vya Mwl.
J. K. Nyerere mjini Morogoro.
Alisema
pamoja na wataalamu wa sekta ya kilimo, ufugaji na uvuvi kujitahidi
kuvumbua teknolojia mpya katika sekta hiyo, bado haiwafikii wananchi wa
vijijini.
Hivyo
amewataka watalaamu hao pamoja na kuongeza jitihada za kuvumbua, elimu
hiyo waipeleke kwa wananchi ili kuondoa umasikini miongoni mwao.
“Kazi
kubwa imefanyika ya utafiti, viwango vimeongezeka sana vya ubora, suala
kubwa ni namna gani uvumbuzi unaofanywa na maabara kwenye vituo vyetu
utawafikia wakulima,” alisema Kikwete.
Alisema
ili kuondokana na umasikini kwa haraka, wataalamu wanatakiwa kutoa
elimu kwa wakulima na wafugaji namna ya kulima na kufuga kibiashara na
kuondokana na dhana ya kufanya kazi hizo kwa kujikimu peke yake.
Mpekuzi.
Comments