Waziri
wa Maliasili na Utalii, Hamis Kigwangala leo anaadhimisha siku yake ya
kuzaliwa akiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili anakotibiwa.
Dk
Kigwangala, leo Agosti 7, anatimiza miaka 43 ya kuzaliwa kwake. Waziri
huyo alipata ajali ya gari Agosti 4 mwaka huu eneo la Magugu, Manyara.
Ameandika katika ukurasa wake wa twitter akimshukuru Mungu kwa kufikisha umri huyo.
“Leo
ninatimiza miaka 43 toka nizaliwe. Ahimidiwe Allah aliye Mkuu kuwa bado
nipo hai mpaka sasa. Najua ni kwa utashi na kusudio lake. Namshukuru na
nazidi kuomba kwake shufaa, siha na mafanikio tele. Ninawashukuruni
nyote kwa dua zenu. Tudumu kwenye sala ndugu zangu.” Ameandika.
Pia, ameutumia mtandao huo, kumkumbuka Ofisa Habari wa Wizara yake, Hamza Temba aliyefariki dunia katika ajali hiyo.
“Sijui
hata Kwa nini usiku huu nimegusa simu? 😭😭😭 Only to look at my phone
and come across chats and pics za ziara yetu ya #PoriKwaPori and rise to
the reality that mdogo wangu, bwashee wangu, this hard working, smart,
handsome and very hopeful young man sintomuona tena na kumtania. What
more can I say?! Alhamdulillah. Qaalu inna lillah wainna ilayhir
rajiuun. 🙏🏿 #AllahAkbar“
Mpekuzi.
Comments