Katibu Mkuu wizara ya Fedha Dotto James awataka watanzania kuchangamkia fursa ya kununua matrekta (TEMCO) Kibaha.
KATIBU
Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James amewataka watanzania
kuchangamkia fursa ya kununua matrekta yaliyopo katika kiwanda cha
kuunganisha matrekta ambacho kinamilikiwa na Serikali kilichopo Kibaha
mkoani Pwani.
Amesema
kuwa matrekta hayo yanaubora wa hali ya juu na kuwahakikishia wananchi
watakaoyanunua matrekta hayo kutokuwa na hofu kwani uingizwaji wake
Serikali inahusika moja kwa moja.
Katibu
James aliyasema hayo Kibaha mkoani Pwani wakati akikabidhi matrekta
kumi kwa Chuo cha kilimo Sokoine (SUA) ikiwa ni utekelezaji wa ahadi I
littles na Rais Dkt.John Magufuli baada ya kufanya ziara chuoni hapo .
Alifafanua
rais alipofanya ziara chuoni hapo alihaidi mambo mawili la kutoa
shilingi bilioni mbili kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi ahadi
ambayo tayari imetekelezwa na jana amekamilisha ahadi ya kukabidhi
matrekta hayo.
”
Ninawataka kwenda kutumia vizuri matrekta haya na kuyafanyia
matengenezo iwapo yatahitaji matengenezo kwani sisi watanzania hatuna
utaratibu wakutuza vitu hata kama tukiona vimeharibika.”alisema James.
Nakuongeza
kuwa” Sisi kama serikali tunachombo maalum cha kufatilia fedha na ahadi
zote ambazo zinatekelezwa ,hivyo hata matrekta haya tutafatilia kuona
yanatumikaje na iwapo mkitumia vizuri na hata kama.mkiomba zingine
tutawapa”alisema James.
Akizungumzia
taasisi hizo za fedha hususani Mfuko wa Pembejeo wa Serikali pamoja na
Benki kuwaeleza wananchi kuwa wanafedha kwa ajili ya kilimo ili waweze
kuchangamkia fursa hiyo.
“Kuna
huu mfuko wa pembejeo ,huu ni mfuko wa serikali kabisa na tunatoa
ruzuku kama ilivyo kwa benki ya kilimo hivyo mjitokeze ili wananchi
wajuwe.” alisema James.
Aliongeza
kuwa Serikali ya Tanzania na Poland zimeingia makubaliano kwa ajili ya
kutengeneza matrekta lengo nikuona tunakuwa na matrekta ya kutosha na
kwakuazi ni kutengeneza matrekta 2400 kwa nchi mzima..
Kwa
upande wake Makamu mkuu wa Chuo cha Kilimo (SUA) Profesa Raphael
Chibunda alimhakikishia Katibu mkuu wa Wizara ya fedha Dotto Kwamba
matrekta hayo watayatumia vizuri huku wakishukuru pia kupewa shilingi
bilioni mbili kwa ajili ya ujenzi wa mabweni.
Alisema
kwakuwa chuo chake ndicho ambacho kinatoa watalaamu wengi kwenye kilimo
hivyo watahakikisha utaalamu huo unawafikia kikamilifu watanzania
kupitia sekta ya kilimo.
Mpekuzi.
Comments