JESHI
la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limetangaza nafasi za
kuandikishwa jeshini madaktari wa binadamu na fani nyingine za tiba.
Taarifa
hiyo imetolewa jana tarehe 31, 2018 na Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano
JWTZ, Kanali Ramadhan Dogoli wakati akizungumza na wanahabari jijini
Dar es Salaam.
“Nafasi
hizo zinatolewa ili kuongeza idadi ya wataalamu wa tiba watakaotoa
huduma za afya katika hospitali zetu, vituo vya afya na Zahanati
kulingana na mahitaji ya sasa na siku zijazo,” alisema Kanali Dogoli.
Alisema
watakao andikishwa Jeshini ni wale wenye taaluma za Doctor of Medicine,
Doctor of dental sugery, bachelor of pharmacy, bachelor in laboratory
science, bachelor of science in nursing, bachelor of science in
physiotherapy na bachelor of science in prosthetics and orthotics.
Kanali
Dogoli ametaja sifa za watu wanaohitajika kuandikishwa ikiwemo, mhusika
awe na umri kati ya miaka 18 hadi 28 na mzaliwa wa Tanzania, awe
hajawahi kupatikana na hatia ya makosa ya jinai mahakamani na kufungwa
jela, awe na cheti halisi cha kuziliwa.
Pia,
kama ni daktari awe amemaliza mafunzo kwa vitendo na kutunukiwa vyeti
pamoja na kusajiliwa na Bodi. Awe hajawahi kutumikia Jeshi la Polisi,
Magereza, Chuo cha Mafunzo au Kikosi Maalumu cha Kuzuia Magendo.
Kanali
Dogoli amesema wenye sifa tajwa na kuhitaji kujiunga na JWTZ waripoti
katika kambi ya Jenerali Abdallah Twalipo, Mgulani Dar es Salaam tarehe
28 Agosti, 2018 kuanzia saa moja asubuhi.
“Watakaochaguliwa
na kuandikishwa jeshini watapatiwa mafunzo mbalimbali ya jeshi na
yatakayo waendeleza katika taaluma zao. Wakiwa Jeshini majukumu
watakayopatiwa ni yale yatakayowapachangamoto na fursa nzuri za kutumia
taaluma zao,” alisema Kanali Dogoli.
Mpekuzi.
Comments