Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.
Selemani Jafo amewataka Wakuu wapya wa Wilaya walioteuliwa hivi karibuni
kuhakikisha wanasoma na kuzielewa sheria zinazowaongoza ili kufanya
kazi kwa weledi.
Mhe.
Jafo aliyasema hayo leo Jijini Dodoma kwenye kikao kazi na Wakuu hao wa
wilaya kwa lengo la kuwapa maelekezo ya kazi ambapo aliwaambia mada kuu
ya kikao hicho ni mahusiano na mawasiliano kazini pamoja na kuhakikisha
kuwa wanafanya kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizopo.
“Msiende
kuwa vyanzo vya migogoro kwenye Wilaya zenu, tumekuwa tukishuhudia
migogoro baina ya Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Wenyeviti wa
Halmashauri, Makatibu Tawala pamoja na Wabunge, hatuwezi kwenda hivi,
katengenezeni serikali” Alisema Waziri Jafo.
Hata
hivyo alikemea tabia ya baadhi ya Wakuu wa Wilaya kuitumia vibaya
mamlaka waliyonayo na kuwaweka watu ndani hali iliyopelekea wananchi
kuichukia serikali yao, hivyo kuwataka kutumia sheria kama iliyokusudiwa
na siyo kwa kuonea watu.
Aidha
aliwataka Wakuu hao wapya wa Wilaya kutoa ushirikiano kwa wale
wanaotekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na siyo vinginevyo
ikiwa ni pamoja kusimamia miradi ya maendeleo ikiwemo uboreshaji wa
miundombinu ya afya na elimu unaoendelea kote nchini.
Kwa
upande mwingine Waziri Jafo amesema “Kasimamieni ukusanyaji wa mapato
ya serikali kupitia mfumo wa kieletroniki sambamba na kudhibiti uvujaji
wa mapato hayo, lakini pia mkadhibiti madeni kwa kuwa fedha hizo ndizo
zinazotegemewa kwa ajili ya maendeleo nchini”.
Naye
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Injinia Mussa Iyombe amewataka
Wakuu hao wa wilaya kuzitendea haki nafasi walizopewa kwa kufanya kazi
kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni zilizopo hasa pale
wanapomuadhibu mtumishi aliyekosea.
“Serikali
ina taratibu zake, baadhi ya wakuu wa wilaya walikuwa wanatia aibu,
kama kuna mtumishi kakosea, tumia mamlaka zinazomuongoza kumshughulikia,
na sio kusimamisha watu kazi hovyo, kutumbua tumbua hovyo” Alisisitiza
Injinia Iyombe.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro kwa niaba ya wakuu
wenzake wa wilaya amesema watahakikisha wanafanya kazi kwa kuzingatia
kasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe
Magufuli.
Mpekuzi.
Comments