Hakikisheni Taarifa Mnazozitoa Wakati Wa Kusajili Kadi Zenu Za Simu Ni Sahihi, Vinginevyo Sheria Itafuata Mkondo Wake.
Mamlaka
ya mawasiliano nchini TCRA imewataka wananchi kufahamu wajibu na haki
zao wanazostahili kupata kutoka kwenye mitandao inayotoa huduma za
mawasiliano sambamba na kutambua wajibu walionao kama watumiaji wa
huduma za mawasiliano
Kaimu
mkuu wa Kanda ya kaskazini Francis Msungu amesema kuwa mamlaka inatoa
elimu kwa wananchi kuzijua haki zao kutokana na mabadiliko yanayotokea
ni mengi ya sayansi na teknolojia pamoja na maendeleo ya matumizi ya
vifaa vya mawasiliano katika mitandao ya simu.
Amesema
kwa sasa kumezuka wimbi la utapeli kupitia simu za mikononi, hivyo
wananchi wametakiwa kuwa na tahadhari kubwa, wasikubali kurubuniwa
katika vitu ambavyowanafahamuhawajashiriki Usitekeleze maagizo yeyote
yahusuyo fedha kwa ujumbe wa maandishi,
"Mfano unatumiwa ujumbe kuwa umeshinda bahati na sibu katika
Mashindano
ambayo hujashiriki, ukipokea ujumbe umetumiwa pesa na mtu usiyemfahamu
usizitoe fedha hizo, hadi uthibitishe ya kwamba zimetumwa kwa nia nzuri"
Amewataka
wananchi mara waonapo fedha imetumwa kwenye mitandao yao na
aliyezituma bado hajafahamika, ni vyema wakawa na subira hadi watakapo
hakikisha zimetumwa kwa nia njema ili wasiingie kwenye matatizo.
"Watu huwa wanakosea pia yamkini zilitumwa kwa bahati mbaya, ukiwahi kuzitoa nawe unahesabika unaiba. "alisema
Amewataka
watumiaji wa simu za mkononi kufahamu kuwa zipo tahadhari za
kuchukuliwa ikiwepo kusajili namba kwa majina kamili ya muhusika kwani
ni takwa la kisheria, bila kusahau kwamba kila taarifa zinazoyolewa
wakati wa usajili ziwe za sahihi.
Taarifa zako zikiwa za uongo hilo nikosa kisheria utapata adhabu ya kifungo au kulipa shilingi milioni 3 au vyote kwa pamoja.
Ameshauri
kwamba yeyote akipoteza simu au kadi atoe taarifa kwa jeshi la polisi
na kwa mtoa huduma, samba na kuchukua tahadhari mara uokotapo simu au
kadi ya simu utoe taarifa kwa usalama wako zaidi
Wananchi
wote wanaotembelea maonyesho 25 ya kilimo na sherehe za nanenane kanda
ya kaskazini mwaka 2018 wanashauriwa kutembelea banda la TCRA ili
waweze kupata elimu zaidi ya mawasiliano.
Mpekuzi.
Comments