Naibu
Katibu Mkuu wa Chadema (Zanzibar), Salum Mwalimu, amesema milango ipo
wazi kwa wabunge na madiwani wa chama hicho wanaokubali kurubuniwa na
kukikimbia chama.
Alisema wabunge na madiwani hao hawana dhamira ya dhati ya kuwatumikia wananchi, hivyo wanaweza kwenda wanakorubuniwa.
Alisema
hayo mwishoni mwa wiki mjini hapa wakati akiwahutubia mamia ya wananchi
katika mkutano wa hadhara wa kumnadi mgombea udiwani wa Kata ya Bagara,
Mathias Zebedayo.
"Kwa
wale wenye njaa watakwenda, kwa wale wasio na hofu ya Mungu watakwenda
na kwa wale ambao walikuwa hawana dhamira ya kweli watakwenda kwa kuwa
walihitaji udiwani na ubunge, lakini wanaohitaji mapinduzi ya kweli
watabaki,'' alisema.
Aidha,
alidai Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilizoea kutumia nguvu za dola
kuwaibia kura wapinzani wakaona mbinu hiyo haitoshi, sasa wameamua
kuanza kuwanunua wabunge na madiwani.
Alisema
Chadema inawaacha wabunge na madiwani wanaokubali kununuliwa ili waende
kushirikiana na watu waliozoea wizi na ufisadi katika majimbo yao na
halmashauri zao na kusababisha huduma za kijamii kukosekana.
Aliwaomba
wakazi hao kumchagua mgombea udiwani wa Chadema ili waendelee kuleta
maendeleo katika halmashauri hiyo kwa kuwa wameshaonyesha njia.
Alisema
kwa mfano, wakati wanaichukua halmashauri walikuta makusanyo kwa mwezi
ni Sh. milioni 700, lakini kwa sasa halmashauri chini ya Chadema
inakusanya Shilingi bilioni mbili ambazo zinasaidia kuwaletea maendeleo.
Akimwombea
kura za ndiyo mgombea wa Chadema, Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini,
Pauline Gekul, aliwataka wananchi kujipanga kulinda kura zao.
"Wale
ambao wamezoea kutuonea kwenye uchaguzi na kutuibia kura zetu awamu hii
tumeandaa wazee wa kimila, ili wakituhujumu kwa njia yoyote wafe mtaona
watakavyolaliana hapa wakifa mmoja baada ya mwingine,'' alisema.
Mgombea
udiwani wa Kata ya Bagara, Mathias Zebedayo, aliwaomba kumchagua ili
aweze kuyaendeleza yale yote aliyoshindwa mtangulizi wake kwa miaka
mitatu iliyopita na kutimkia CCM.
Mpekuzi.
Comments