Askari
mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) anashikiliawa na jeshi
la polisi Mkoani Morogoro kwa tuhuma za kukodisha silaha kwa wahalifu
zinazotumika kwenye matukio ya ujambazi.
Akizungumza
jana Agosti 14, kamanda wa polisi mkoani Morogoro, Wilbroad Mutafungwa
alisema watuhumiwa 39 wa matukio hayo walihusishwa kwenye matukio ya
uhalifu ikiwamo kukutwa na silaha za aina tano, bangi kete 200, bangi
misokoto 66, risasi 27, pamoja na pombe aina ya gongo lita 58.
Mtuhumiwa
Lumi Guya maarufu kama Mbulu (67) mkazi wa Kingolwira alikamatwa kwa
tuhuma za kukodisha silaha yake aina ya Shot Gun anayoimiliki kihalali
kwa watu wanaofanya uhalifu.
Kamanda
huyo amesema mtuhumiwa huyo ni mwanajeshi mstaafu wa JWTZ na
hushirikiana na Miraji Jumanne(28)mkazi wa Kichangani ambaye inadaiwa
aliwahi kuwa askari polisi na kufukuzwa kutokana na vitendo visivyofaa
wakishirikiana na wenzao sita ambao wote wanashikiliwa.
Watuhumiwa
wengine walikamatwa katika matukio ya wizi, uuzaji gongo, wafugaji
kulisha mifugo kwenye mashanmba ya wakulima na wizi wa kutumia silaha.
Mpekuzi.
Comments