Alichoandika Msemaji Mkuu wa Serikali Baada ya Ubalozi wa Marekani Kudai Uchaguzi wa Marudio Buyungu Ulikuwa na Kasoro.
JANA
Ubalozi wa Marekani ulichapisha tamko lao kuhusu uchaguzi wa marudio
uliomalizika August 12, katika Kata 79 na Jimbo la Buyungu ambapo Mbunge
wake alifariki.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa uchaguzi huo uligubikwa na matukio ya fujo na ukiukwaji wa kanuni za uchaguzi.
Walitoa mfano kitendo cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kushindwa kuwasajili baadhi ya wagombea wa upinzani.
Pia wameguswa na vitisho vilivyotolewa na Jeshi la Polisi kwa Wagombea na wanachama wa vyama vya upinzani ikiwemo pamoja na kukamatwa kwa wagombea na kuzuia mikutano ya kampeni.

Muda
mfupi baada ya taarifa hiyo kusambaa Msemaji wa Serikali Dr. Hassan
Abbas amesema Serikali inajiridhisha juu ya taarifa hiyo na watatoa
tamko lao punde.
“Kuna
taarifa inasambaa kuhusu kinachodaiwa ni taarifa ya ubalozi mmoja
kuhusu masuala ya ndani ya nchi. Tunajiridhisha. Tutatoa tamko punde” Msemaji Mkuu wa Serikali
Mpekuzi.
Comments