Alisema hayo katika kikao cha Pamoja na jumuiya za wenye gari za biashara, katika ukumbi wa Tume ya Ukimwi,Chake Chake.
Alisema sekta ya usafiri ni mihimu katika utoaji huduma na imechangia kwa kiasi kikubwa kutoa ajira kwa vijana.
Aidha alipongeza jihudi zinazochukuliwa na maderena na trafiki katika kupunguza ajali za barabarani kisiwani Pemba.
“Elimu zaidi inahijatika kwa vijana wadogo ambao wameinukia kwa wingi kuendesha vyombo, tunataka kumaliza kabisa tatizo la ajali za barabarani,” alisema.
Aliwaomba viongozi taasisi za usafiri Pemba, kufanya mazungumza na madereva ili kuweza kupunguza mwendo kasi ambao ndio chanzo kikuu cha ajali.
Ali Mohamed Shela mjumbe wa bodi ya usafiri Zanzibar, alisema kituo cha daladala cha sokoni Chake Chake, ni kikwazo kikubwa kwao na baraza la mji huo limeshindwa kukifanyia matangenezo.
Alisema kikwazo chengine ni maegesho ya gari katika mji wa Chake Chake, hali inayosababisha madereva kuegesha gari kando ya barabara kuu.
Zanzibarleo.
Comments