White House yalegeza kamba kuhusu matamshi ya vitisho ya Trump dhidi ya Iran.

White House yalegeza kamba kuhusu matamshi ya vitisho ya Trump dhidi ya IranMsemaji wa Ikulu ya Marekani (White House) amelegeza kkamba kuhusiana na matamshi ya vitisho ya Rais Donald Trump dhidi ya Iran.

Katika radiamali yake kuhusiana na ujumbe tata wa Twitter wa Trump dhidi ya Iran, Sarah Huckabee Sanders amesema kuwa, rais huyo wa Marekani hakukusudia kushadidisha mvutano kati ya Iran na nchi yake. 

Sanders ameongeza kwamba, Trump pia hakukusudia kupotosha kadhia ya mkutano wake tata wa hivi karibuni kati yake na Rais Vladmir Putin wa Russia uliofanyika huko Helsinki, mji mkuu wa Finland. 

Hii ni katika hali ambayo wajumbe wa kamisheni ya masuala ya kigeni katika Bunge la Marekani pia, sambamba na kuukejeli ujumbe wa hivi karibuni wa Trump dhidi ya Iran, wamenukuliwa wakisema kuwa, Marekani haiwezi kuishambulia Iran, ingawa Russia iliweza kuishambulia nchi hiyo katika uchaguzi wa 2016.
Katika jumbe zao, wawakilishi hao waliandika katika kukejeli ujumbe wa Rais Donald Trump aliouandika kwa herufi kubwa dhidi ya Iran kwamba: 
'Usituhadae kwa maandishi yako yote kwa herufi kubwa, sisi hatupo tayari kuishambulia Iran.' Hivi karibuni Trump alitoa matamshi ya vitisho kufuatia indhari aliyoitoa Rais Hassan Rouhani wa Iran kwa Marekani akisema kuwa, "Katu Usitoe vitisho tena kwa Marekani".  
Akizungumza hivi karibuni Rais Rouhani alisema: "Rais wa Marekani anatakiwa kufahamu kwamba, Iran imekuwa ikidhamini amani katika njia za majini katikka eneo katika kipindi chote cha historia, hivyo Trump hatakiwi kucheza na mkia wa simba, kwa sababu jibu la Iran litampelekea ajute."
parstoday.

Comments