Serikali
kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
imewaagiza viongozi wa Mkoa wa Mara na Wilaya ya Musoma kuchunguza
tuhuma zinazohusisha kumbi za starehe wilayani humo kuruhusu watoto
walio chini ya miaka 18 kuingia na kutumia vilevi ndani ya kumbi hizo.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile ametoa agizo hilo alipotembelea Mkoa wa Mara katika
ziara ya kikazi ambapo alipokea malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu
kuwepo kwa kumbi za starehe zinazowaruhusu watoto walio chini ya umri wa
miaka 18 na kutumia pombe wakiwa ndani ya kumbi hizo.
Dkt.
Ndugulile amesema kwamba wamiliki wa kumbi hizo wanakiuka sheria ya
mtoto, hivyo wanapaswa kuchukuliwa hatua za kisheria mapema iwezekanavyo
ili kuwalinda watoto hato chini ya umri wa miaka 18.
Aidha
kwa mujibu wa wa kifungu cha 17 cha Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009
kinasema mtu ambaye ni mmiliki au anayeendesha au ni msimamizi wa ukumbi
wa muziki, 'Bar', au klabu ya usiku hatamruhusu mtoto kuingia katika
maeneno yao.
Katika
kifungu imeelezwa kuwa "mtu atakayekiuka kifungu hiki atakuwa ametenda
kosa na atakapotiwa hatiani atalipa faini ya kiasi kisichopungua
Shilingi millioni moja na kisichozidi Sh millioni tano au kifungo
kisichozidi miezi 12 au vyote kwa pamoja".
Baada
ya agizo hilo kutoka wizarani, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Bw. Adam Malima
amesema ataendelea kuwachukulia hatua wale wote wanaofanya vitendo hivyo
pamoja na kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia, ndoa na mimba
za Utotoni ambazo zinashamiri katika mkoa huo.
Mpekuzi.
Comments