WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imelitangaza zao la michikichi
kuwa zao kuu la sita la biashara linalotarajiwa kuinua uchumi Taifa.
Awali,
kulikuwa na mazao makuu matato ya biashara nchini ambayo ni korosho,
tumbaku, pamba, kahawa na chai, ambayo yanategemewa na Taifa kukuza
uchumi.
Waziri
Mkuu aliyasema hayo jana (Jumapili, Julai 29, 2018) wakati akizungumza
na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya
Mwakizega wilayani uvinza mkoani kigoma.
Alisema
baada ya Serikali kupata mafanikio katika mazao ya korosho, tumbaku,
pamba, kahawa na chai, sasa imeamua kufufua zao la michikichi mkoani
Kigoma ili lianze kuzalishwa kwa wingi na kuongeza pato la serikali.
“Tulianza
na mazao matano, baada ya wakulima wake kupata faida sasa tumehamia
katika mazao mengine likiwemo la michikichi,” alisema.
Waziri
Mkuu aliongeza kuwa Serikali imeamua kulipa kipaumbele zao hilo kwa
lengo la kumaliza tatizo la upatikanaji wa mafuta ya kula nchini.
Alisema
kwa mwaka Serikali inatumia zaidi ya sh. bilioni 600 kuagiza mafuta ya
kula nje ya nchi, hivyo ufufuaji zao hilo utaliwezesha Taifa kuzalisha
mafuta ya kutosha.
Waziri
Mkuu aliwaagiza wananchi wa mkoa wa Kigoma kuandaa mashamba ya kupanda
michikichi wakati Serikali ikipanga namna ya kuwasambazia mbegu.
Pia
aliwaagiza wananchi wote wapande michikichi mbele ya nyumba zao kama
mapambo ambayo baada ya miaka mitatu itageuka na kuwa chanzo cha mapato.
Katika
hatua nyingine, Waziri Mkuu alitembelea na kukagua shamba jipya la
michikichi la kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) 821 KJ Bulombora.
Akiwa
katika shamba hilo jipya lenye ukubwa wa ekari 34, Waziri Mkuu alipata
fursa ya kupanda mche wa mchikichi kwa lengo la kuhamasisha kilimo cha
zao hilo.
Alisema
Serikali itahakikisha inafuatilia kwa ukaribu kilimo cha zao hilo
kuanzia hatua za awali za utayarishaji wa shamba hadi upatikanaji wa
pembejeo.
Kadhalika,Waziri
Mkuu aliwaagiza wazazi kuwakatia vijana wao maeneo kwa ajili ya kilimo
cha michikichi, jambo litakalowakwamua kiuchumi badala ya kuwa tegemezi.
Pia
aliwashauri vijana hao na wakulima wengine wajiunge katika vikundi
vitakavyowawezesha kupata mikopo na kuendeleza mashamba yao ya
michikichi.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
Mpekuzi.
Comments