WAZIRI
Mkuu Kasimu Majaliwa amemuagiza Naibu Waziri wa Kilimo, Bw. Omary
Mgumba afuatilie sh. milioni 150 walizotakiwa kulipwa wakulima wa kahawa
wa chama cha msingi cha Kalinzi Organic Coffee Grower zilizolipwa
kwenye kikundi kingine.
Ametoa
maagizo hayo jana (Jumatatu, Julai 30, 2018) wakati alipotembelea
shamba la kahawa katika kata ya Nyarubanda Wilayani Kigoma, akiwa
njiani kuelekea wilaya ya Buhigwe kwa ajili ya kuendelea na ziara yake
ya kikazi mkoani Kigoma.
Ametoa
metoa agizo hilo baada ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Peter Serukamba
kumuomba awasaidie kutatua changamoto ya malipo ya wakulima wa chama
Kalinzi Organic Coffee Grower ambayo hayajalipwa baada ya kuuza kahawa
yao katika chama cha kahawa moshi miaka saba iliyopita.
Waziri
Mkuu amesema wakulima hao wanatakiwa kulipwa fedha zao kwa wakati,
hivyo amemuagiza Waziri Mgumba kuhakikisha anafuatilia ni kwanini fedha
hizo zililipwa kwa wakulima wa kikundi kingine. Pia ahakikishe wakulima
hao wanapata haki yao.
Hata
hivyo, Waziri Mkuu amewaomba wakaulima hao kupanda miche mipya na
kuachana na ya zamani kwa kuwa uzalishaji wake ni mdogo na inashambuliwa
sana na magonjwa ukilinganisha na miche ya kisasa.
Aidha,
Naibu Waziri huyo wa Kilimo Omary Mgumba alikiri kuwepo kwa mgogoro huo
na ni kweli kuwa fedha hizo zililipwa kimakosa na Bodi ya Kahawa kwenda
kwa chama cha Msingi cha Kalinzi Farm Coffee badala ya chama cha
Kalinzi Organic Coffee Grower. Ameahidi kufuatilia suala hilo.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa Kalinzi Organic Coffee Grower , Bw. Said
Mchachu alisema chama chao kina wakulima 447 ambao tangu wapeleke kahawa
yao Moshi mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya kuiuza mwaka 2012 mpaka sasa
wanaendelea kufuatilia madai yao bila mafanikio.
Alisema
madai hayo yamesababisha migogoro ndani ya chama chao kufuatia baadhi
ya wakulima wakiwatuhumu viongozi kuwa wao ndio wamekula fedha zao jambo
ambalo si kweli, hivyo alimuomba Waziri Mkuu kuwasaidia ili waweze
kupata fedha zao.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
Mpekuzi.
Comments