Waziri
wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amesema hatasita kufuta makanisa au
misikiti inayoshindwa kutatua migogoro ya taasisi hizo.
Ametoa kauli hiyo jana Julai 29, 2018 katika Kanisa la Pentekoste la Leganga, lililopo Arumeru mkoani Arusha.
“Kuanzia
sasa, kanisa lolote au msikiti wowote utakaokumbwa na migogoro na
kushindwa kuitatua wenyewe; misikiti hiyo, makanisa hayo nitakwenda
kuyafuta mara moja,” alisema.
Alisema hatua hiyo inalenga kuhakikisha yanakuwapo makanisa na misikiti inayohubiri amani na utulivu.
Waziri
Lugola ameonya askari Polisi wanaowashusha jukwaani masheikh na
wachungaji inapofika saa 12:00 jioni, akisema muda huo ukifika
waimarishe ulinzi ili waumini wamalize ibada zao vizuri.
Mpekuzi.
Comments