Hayo aliyaeleza alipokuwa akizindua kamati maalum ya maandalizi na
usimamizi wa Tamasha la Maonyesho ya Kitalii Zanzibr 2018, Kikwajuni
mjini Unguja jana.
Alisema kupanuka kwa soko hilo kutawawezesha watalii wengi zaidi
kuingia nchini na hivyo kuongeza mapato sambambamba na kuinua uchumi
kupitia sekta ya utalii.
Aidha, alisema, tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika kuanzia Oktoba
17 hadi 20, litapewa uzito mkubwa kwa lengo la kuhakikisha linavuta
idadi ya wageni na kuitangaza Zanzibar kimataifa.
“Hayo yanayofanyika ni miongoni mwa mikakati ambayo inalenga
kiimarisha sekta ya utalii kwa manufaa ya nchi na wananchi wake kwa
ujumla”, alisema.
Alisema lengo la tamasha hilo ni kuwaleta wadau wa utalii nchini
badala ya kwenda nje kuitangaza Zanzibar kama ambavyo imekuwa ikifanyika
huko nyuma.
Wajumbe wa kamati hiyo ni Dk.Vuai Iddi Lila(Mwenyekiti), Javed
Jafferji (Makamu), Dk.Juma Mohammed Salum (Mjumbe), Shariff Ali Shariff
(mjumbe), Hassan Ali Mzee (Mjumbe), Julia Bishop (Katibu wa Kamati),
Mohammed Mbwana Mkadara (Mjumbe) na Nicolas Chedro (Mjumbe).
Zanzibarleo.
Comments