Jeshi
la Polisi Mkoani Kilimanjaro limetakiwa kujitathmini baada ya
malalamiko kutoka kwa wananchi kuwa kuna baadhi ya askari polisi
wanajihusisha na vitendo vya kudai rushwa.
Kauli
hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira kwenye
hafla iliyoandaliwa na Kamanda wa Polisi wa Kilimanjaro Kamishna
Msaidizi wa Polisi, Hamisi Issa kwa ajili ya kufahamiana, kujenga na
kuimarisha mahusiano kati ya Jeshi hilo na vyombo vingine vya umma na
sekta binafsi.
Amesema kuwa vitendo hivyo vimekuwa vikichafua taswira ya Jeshi la Polisi kutokana na baadhi ya askari kutenda makosa hayo.
“Nimekuwa
nikipokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi juu ya vitendo vya
rushwa na wakati mwingine nililazimika kumueleza Kamanda wa Polisi wa
Mkoa wa Kilimanjaro Kamishna Msaidizi wa Polisi, Hamisi Issa ili
alishughulikie suala hilo,”amesema Mghwira
Hata
hivyo, Julai 21, 2018, Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola ambaye
anasimamia vyombo vya ulinzi nchini pia alionya vitendo vya Jeshi la
Polisi kuwabambikizia wananchi makosa na kuwalazimisha kutoa rushwa huku
akiwataka Watanzania watoe taarifa kwa vyombo husika kwa askari yoyote
ambaye atafanya vitendo hivyo.
Mpekuzi.
Comments