Rais Magufuli Kuongoza Mkutano Mkubwa wa Kisiasa Duniani Unaoratibiwa na Chama cha kikomunisti cha China (CPC).
Rais
John Magufuli anatarajiwa kuongoza mkutano wa vyama vya siasa vyenye
mlengo wa kijamaa utakaofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Julai 17,
mwaka huu.
Mkutano
huo pia utashirikisha viongozi wa mataifa mbalimbali akiwamo Waziri wa
Mambo ya Nje wa China, Wang Yi ambaye atawakilisha Chama cha kikomunisti
cha nchi hiyo (CPC).
Wengine
watakaoshiriki katika mkutano huo ni viongozi wa vyama vilivyopigania
uhuru na ukombozi wa Bara la Afrika na Kusini mwa bara hilo, vikiwamo
vyama vya Frelimo, ANC ,ZANU PF na vinginevyo.
Mkutano
huo ni wa pili kufanyika Duniani, ambapo wa kwanza ulifanyika Beijing,
China Desemba mwaka jana, ambapo Rais wa nchi hiyo, Xi Jinping
alihudhuria na kuziasa nchi za Afrika kuleta maendeleo.
China
ni miongoni mwa nchi zilizo mstari wa mbele kusaidia nchi za Afrika
ikiwamo Tanzania katika kuhakikisha kuwa nchi hizo zinapiga hatua za
kimaendeleo katika nyanja mbalimbali za kisiasa, kiuchumi na kijamii,
hali ambayo inaweza kuwasaidia kuondoka kwenye utegemezi.
Miongoni
mwa miradi iliyotekelezwa na China kwa upande wa Tanzania ni pamoja na
ujenzi wa reli, barabara na kwenye miradi mingine ya kimaendeleo na
kimkakati.
Hivyo
basi katika mkutano huo, wadau wataweza kubadilisha mawazo na uzoefu na
kujenga taswira mpya ya kimaendeleo kupitia vyama vya siasa na kuandaa
mikakati mipya katika utekelezaji wa majukumu yao.
Hata
hivyo katika mkutano huo, pamoja na mambo mengine, Rais Magufuli
ataongozana na Waziri Wang Yi kwa ajili ya kuweka jiwe la jiwe la Msingi
la ujenzi wa Chuo Cha Uongozi Cha Chama Cha Mapinduzi(CCM)
kitakachojengwa Kibaha mkoani Pwani.
Chuo
hicho kitaanza kutoa mafunzo mwaka 2020 ambapo, wanafunzi kutoka nchi
zilizopigania uhuru na ukombozi wa Bara la Afrika watapata mafunzo.
Mpekuzi.
Comments