Akizungumza na Zanzibar Leo, Ofisa Uhusiano wa Idara hiyo, Mlalama
Amlima, alisema raia huyo aliingia nchini Julai 17 akiwa kwenye mavazi
ya kike wakati hati yake ya kusafiria ikionesha ni mwanamme.
Alisema ndipo walipoamua kumpekua ili kubaini jinsia yake ndipo walipogundua kwamba ni mwanamme.
Alimtaja Mtaliana huyo kuwa ni Davide Katena (46), ambae alikuwa aingie nchini kwa ajili ya kufanya ‘show’.
“Tulimkagua na tulipojiridhisha kwamba ni mwanamme tukamzuia kuingiza
nchini kwa sababu kitendo alichofanya ni kinyume na maadili ya
Zanzibar,” alisema.
Hata hivyo, alisema hiyo si mara ya kwanza kwa maofisa uhamiaji
katika uwanja huo kuwarejesha walikotoka wageni wanaokiuka silka,
maadili na utamaduni wa Zanzibar.
Picha zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijanii zinamuonesha mtalii
huyo akiwa amevalia kazu ya rangi ya zambarau, viatu vya kike na nywele
ndefu vitu ambavyo vinamtambulisha kama mwanamke kwa kumungalia.
Zanzibarleo.
Comments