Mkurugenzi
wa halmashauri ya Mtwara, Omari Kipanga, amekiri kupata nakala ya barua
ya kujitoa kwa Mgombea wa nafasi ya Udiwani katika Kata ya Muungano,
halmashauri ya Wilaya ya Mtwara.
Mkurugenzi
huyo amepokea barua hiyo ya mgombea udiwani kupitia Chama cha
Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Ismail Liuye jana ikiwa ni siku chache
zimesalia kabla ya kufikia uchaguzi mdogo wa marudio unaotarajiwa
kufanyika Agosti 12 mwaka huu.
Taarifa
zinaeleza kuwa Bw. Liuye amejitoa katika kinyang'anyiro hicho baada ya
kupokea vitisho kwa kutoka kwa watu mbalimbali kwa njia ya ujumbe mfupi
wa maandishi, akitishiwa maisha yake pamoja na familia yake.
Hata hivyo baada ya kuzungumza na bwana Liuye amedai kwamba ameamua kuacha kutokana na kwamba ni uamuzi wake.
"Mimi siendelei na kampeni, nimeacha. Nimeacha tu. Mtu unapoamua kuacha kitu si unaacha tu. Sababu nilizonazo ni za kwangu binafsi. Kama inasemekana kuhusu kutishiwa iendelee kusemekana".Amesema
"Mimi siendelei na kampeni, nimeacha. Nimeacha tu. Mtu unapoamua kuacha kitu si unaacha tu. Sababu nilizonazo ni za kwangu binafsi. Kama inasemekana kuhusu kutishiwa iendelee kusemekana".Amesema
Hata
hivyo Mkurugenzi wa Itifaki na Mawasiliano ya Mambo ya Nje wa CHADEMA,
John Mrema amesema kwa sasa bado hana taarifa za kuhusu kujiondoa kwa
mgombea wao katika kinyang'anyiro hicho na kwamba anachoamini kampeni
zilikuwa zikiendelea labda awe amejiondoa baada ya Kampeni za jana na
kwamba bado anafuatilia habari hizo.
Pamoja
na hayo Mkurugenzi Kipanga ameeleza kutokana na muda wa kuweka wagombea
kupita, mgombea wa nafasi hiyo kupitia CCM, Hassan Likuto, atapita bila
kupingwa kutokana na kutokuwapo kwa mgombea wa Chama kingine hivyo
wanachosubiri ni taratibu za Tume waweze kumtangaza Likuto.
Hata hivyo amesema uchaguzi bado unaendelea katika Kata nyingine mbili zilizosalia.
Mpekuzi.
Comments