
Kwa mujibu wa taarifa aliyosambaza kwenye vyombo vya habarin leo
Julai 19, Mwidau ameeleza sababu ya kuhama CUF akidai anajipanga
kivingine katika safari ya kuwaletea maendeleo wananchi.
Amesema amechukua uamuzi huo ikiwa ni miaka miwili na nusu ya
kutafakari mwenendo wa kisiasa ndani ya CUF vyama vingine vya
upinzania pamoja na utendaji wa Serikali ya awamu ya tano na hivyo
ameamua kujivua.
“Nimeridhika sasa ni wakati muafaka wa kujipanga kivingine
katika safari ya kushiriki kuleta maendeleo na ustawi wa wananchi wote,”alisema Mwidau.
Mwidau aliyekuwa mbunge kuanzia wa viti maalum 2010 hadi 2015 pia
aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya bunge ya Hesabu za Serikali(PAC)
amesema ameamua kujiunga na CCM kwa sababu bado anayo ndoto ya
kuendelea kushirikiana na wananchi wote katika kuleta ustawi na
maendeleo na hayupo tayari kuishia njiani.
Akizungumza jana, katibu wa CCM, Mkoa wa Tanga, Allan Kingazi amesema
kuwa mapokezi ya Mwidau yatafanyika Jumamosi katika uwanja wa Makorora
Katim.
“Tutampokea kesho jumamosi Makorora jijini Tanga tumefurahi kwa sababu Mwidau ana nguvu hasa kwenye siasa za Wilaya ya Pangani.”alisema Kingazi.
zanzibar24.
Comments