Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe ameagiza
uongozi wa chama hicho kila wilaya kujenga ofisi ifikapo mwaka 2020 na
kuondokana na adha ya kupanga.
Ametoa
agizo hilo wakati akiweka jiwe la msingi katika jengo la ofisi ya
Chadema wilayani Tarime mkoani Mara, ambapo amesisitiza kuwa mpango wa
ujenzi wa ofisi hizo ulicheleweshwa na huo haukuwa muda wake.
“Mpango
wa ujenzi wa hili jengo umecheleweshwa na huu haukuwa muda wake lakini
nawapongeza viongozi walioona njozi ya kuanzisha ujenzi huu ambao uko
hatua ya renta ili kuunga mkono ujenzi huu Mimi naanza na Shilingi
milioni mbili kila mbunge mkoani Mara achangie milioni moja,”amesema
Mbowe
Juzi,
aliyekuwa mbunge wa jimbo la Ukonga kupitia chama hicho, Mwita Waitara
alimtuhumu mwenyekiti huyo kuwa hela za ruzuku za chama hicho
hazieleweki zinakwenda wapi, huku chama hicho kikiwa hakina ofisi makao
makuu, Kanda wala mikoani.
Mbowe
ametoa maagizo hayo wilayani humo ambapo amekwenda kwaajili ya uzinduzi
wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Turwa.
Mpekuzi.
Comments