Akizungumza na gazeti hili ofisini kwake Malindi, Ofisa Uhusiano wa
baraza hilo, Hassan Yahaya Hassan, alisema vikundi hivyo ambavyo
vitakuwa na watu takribani ya 200 vitafanya kazi hiyo kwa muda wa mwaka
mmoja kwa mujibu wa vigenzo na masharti waliokubaliana.
Alisema wameamua kuwashirikisha wananchi katika kufanya usafi ili kuuweka mji katika hali ya usafi.
Alisema wameamua kufanya hivyo kwa sababu wananchi ndio walengwa wakuu na ndio waathirika pale yanapotokea maradhi.
Maeneo ambayo yanatarajiwa kufanyiwa usafi ni pamoja masoko, maeneo
yote ya barabara za manispaa ya mjini, kwenye michirizi ya maji ya mvua,
uzibuaji wa maji ya machafu na maeneo ya bustani.
Alisema kwamba wameamua kufanya hivyo kutokana na kutokuwa na wafanyakazi wa kutosha wa kufanya kazi hiyo.
Alitumia fursa hiyo kuiomba jamii kushirikiana na vikundi hivyo ili kudumisha usafi katika maeneo yote.
Zanzibarleo.
Comments