Kangi Lugola amtimua Kamishna Mkuu wa Magereza, Juma Malewa ....Ni Baada ya Kuchelewa Kwenye Kikao kwa Dakika 1.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola, amemfukuza kikaoni Kamishna Mkuu wa Magereza, Juma Malewa kwa kuchelewa.
Lugola amemfukuza Dk Malewa leo Julai 6, saa tano asubuhi ikiwa ni dakika chache baada ya kikao hicho kuanza.
Awali,
Lugola alisema ikifika saa 5 kamili, mlango ufungwe na kama
alivyoagiza, ulifungwa. Ilipofika saa 5:1 mlango ulifunguliwa ili Dk
Malewa aingie.
Baada ya kuingia Dk Malewa, Lugola akahoji kwa nini amefunguliwa mlango?
Licha
ya Dk Malewa kuomba msamaha, Lugola alikataa kata kata. Pia Lugola
ameagiza Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani, kumshusha cheo hadi
kubaki na nyota tatu, mkuu wa usalama barabarani, Mbeya, Leopold Fungu.
Pia ameagiza Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto mkoa wa Kagera, George Mrutu ashushwe cheo.
Kikao hicho ni cha kimkakati cha viongozi wa vyombo na taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo.
Mpekuzi.
Comments