Chama
cha Wananchi (CUF) kimesema mwenyekiti wa kamati ya uongozi ya chama
hicho, Julius Mtatiro amekamatwa na Polisi kutokana na ujumbe alioutuma
katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa facebook unaodaiwa
kumkejeli Rais John Magufuli.
Naibu
Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano ya Umma wa chama hicho,
Mbarala Maharagande katika taarifa yake kwa vyombo vya habari amesema
Mtatiro amekamatwa jana Julai 5, 2018 na hadi sasa anashikiliwa na
polisi.
Amesema mwenyekiti huyo katika ukurasa wake wa mtandao wa facebook ameandika, ‘rais kitu gani bwana’.
“Juzi
Mtatiro alipokea simu ya wito wa kuhitajika kituo kikuu cha polisi Dar
es Salaam. Jana alikuwa amealikwa kama mmoja wa wageni wawezeshaji wa
mjadala na taasisi ya Twaweza katika kongamano la kujadili maoni ya
wananchi kuhusu kushiriki maandamano na siasa,” amesema Maharagande.
“Ilipofika
saa tatu asubuhi akiwa anaelekea huko alipigiwa simu kujulishwa afike
kituoni hapo saa nne asubuhi. Niliambatana naye mpaka kituoni hapo na
tulipokelewa na ZCO na kujulishwa kuwa anahitajika achukuliwe maelezo
yake kuhusu ujumbe alioutuma katika mtandao huo.”
Amesema,
“Tukakabidhiwa maofisa wa polisi wa kufanya kazi hiyo. Wakati wa kuanza
kuchukuliwa maelezo yake alielezwa kuwa anatuhumiwa kwa kutuma ujumbe
wa kejeli na kashfa dhidi ya Rais Magufuli kupitia mtandao wa kijamii.”
Amebainisha
kuwa mwenyekiti huyu wa CUF upande unaomuunga mkono Katibu Mkuu wa
chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad, alichukuliwa maelezo hadi saa 10
jioni, baadaye kuelekea nyumbani kwake kwa upekuzi.
Amesema
walirejea tena kituoni hapo saa 4 usiku na maofisa wa polisi
walimueleza kuwa wataendelea kuwa naye mpaka leo asubuhi, “Walisema
watatujulisha kama watampatia dhamana au vinginevyo.”
Amebainisha kuwa Mtatiro amewataka wanachama wa CUF kutokuwa na hofu juu yake, wajitokeze kwa wingi mahakamani.
Mpekuzi.
Comments