Wakuu
wa mikoa sita jana, walikuwa miongoni mwa wageni walioipokea ndege mpya
aina ya Boeing 787-8 kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwanza.
Wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mangola wakuu wa mikoa walishuhudia ndege hiyo ya kisasa, ikitua kwa mara ya kwanza mjini hapa saa 4:19 asubuhi ikiwa na abiria 255.
Wakuu
wa mikoa hiyo, Adam Malima (Mara), Mhandisi Robert Gabriel (Geita),
Zainabu Tarack (Shinyanga), Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu (Kagera)
na na Anthony Mtaka (Simiyu) na viongozi dini
Akizungumza
wakati wa mapokezi ya ndege hiyo,Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwele alisema Serikali ina mpango wa
kuboresha majengo ya abiria na mizigo ikiwa ni pamoja na upanuzi wa
viwanja vya ndege nchini.
Alisema
baada ya kuanza upanuzi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere,Uwanja wa Ndege wa Songwe, sasa wametenga fedha kwa ajili ya
uwanja wa ndege wa Mwanza.
Alisema
uwanja wa Mwanza ndiyo mrefu kuliko viwanja vyote, ukiwa na urefu wa
kilomita 3.9, kubainisha kwamba ujio wa ndege mpya aina ya Boeing 787-8
(Dreamliner) utakuwa kichocheo kikubwa cha uchumi na maendeleo.
Naye
Mongela alisema safari ya Mwanza kwenda Dar es Salaam kupitia
Kilimanjaro kwa ndege, ni muhimu hivyo huduma ujio wa ndege ni muhimu
sana kwa wakazi wa Mwanza na mikoa jirani.
Comments