Sayyid Kamal Kharrazi Waziri wa zamani wa Mashauuri ya Kigeni wa Iran ambaye yuko safarini nchini Ujerumani amesema katika mazungumzo yake na Norbert Röttgen, Mkuu wa Kamisheni ya Siasa za Kigeni ya Ujerumani na kuongeza kuwa, Iran imekuwa na nafasi muhimu mno katika kuleta amani na uthabiti Mashariki ya Kati.
Mkuu wa Baraza la Kistratijia la Uhusiano wa Nje wa Iran amesema bayana kwamba, mataifa ya eneo hili pia yanapaswa kufanya mazungumzo baina yao na kuleta amani na uthabiti wa eneo hili bila ya kuingiliwa na madola ya kigeni.
Dakta Kamal Kharrazi ameongeza kuuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iko tayari kufanya mazungumzo na nchi za eneo na kwamba, endapo kutakuwa na irada sahihi na ya kweli mazungumzo hayo yanaweza kuwa na natija.
Kwa upande wake Norbert Röttgen, Mkuu wa Kamisheni ya Siasa za Kigeni ya Ujerumani ameashiria migogoro na matukio ya Mashariki ya Kati na kusema kuwa, hakuna wakati ambao eneo hili lilikabiliwa na machafuko kama ilivyo hii leo, hivyo kuna haja na udharura wa nchi za eneo hili kuchukua hatua za maana ili kudhibiti hali hii.
Comments