Chama
Cha Mapinduzi kimetangaza kuvuna wanachama 170 wa upinzani wilaya ya
Moshi vijijini mkoani Kilimanjaro, huku kikijigamba kwamba tukio hilo ni
ishara ya kuvunja ngome ya Mbunge wa Vunjo, James Mbatia (NCCR-
Mageuzi).
Mbatia
aliibuka mshindi katika uchaguzi wa mwaka 2015 na kuwabwaga, washindani
wake wa karibu, Innocent Melleck Shirima (CCM) na Augustino Mrema
(TLP).
Wanasiasa hao wamedaiwa kupokelewa na Katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Jonathan Mabihya katika kata ya Njiapanda Mashariki.
Wanachama
wanaodaiwa kutoka vyama vya Chadema, NCCR-Mageuzi pamoja na CUF katika
mkoa huo.Akizungumza baada ya kuwapokea wanachama hao na kuwapa kadi za
CCM, Mabihya aliwapongeza kwa maamuzi waliyochukua.
Kwa
upande wake, Katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya Moshi vijijini, Hussein
Jamal alisema wilaya hiyo ina majimbo mawili ya Vunjo na Moshi vijijini.
Mpekuzi.
Comments