Agizo La Rais Magufuli Kuhusu Fedha Za Mashujaa Kutumika Kuboresha Miundombinu Ya Barabara Latekelezwa.
Mnamo
mwezi Juni, mwaka 2018, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Kassim Majaliwa alitoa taarifa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, ameagiza) fedha zilizokuwa
zimetengwa kwa ajili ya kumbukumbu ya siku ya Mashujaa kiasi cha
Shilingi milioni 308, zitumike kuboresha miundombinu ya barabara
jijini Dodoma.
Kufuatia
agizo hilo, Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA), walipata
kiasi cha Shilingi milioni 288 kwa ajili kuweka taa 57 kwenye barabara
ya Emmaus-African Dream na taa 42 kwenye barabara ya Kisasa. kiasi cha
shilingi milioni 20 walipewa Wakala wa Barabara Dodoma (TANROADS), kwa
ajili ya kuhamisha taa ya kuongoza magari kutoka njia panda ya Area D na
kuwekwa kwenye makutano ya barabara ya Emmaus.
Tayari
TARURA wameanza kutekeleza agizo hilo kwa kuweka taa kwenye barabara ya
Kisasa na Emmaus-African Dream. Kwa upande wa TANROADS-Dodoma, zoezi la
kuhamisha taa ya kuongoza magari limetekelezwa, ambapo wakandarasi
watakabidhi kazi hizo rasmi mwezi Agosti mwaka huu.
Akiongea
wakati wa ukaguzi wa kazi hiyo katika barabara ya Emmaus-African Dream
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa Faustin
Kamuzora alifafanua kuwa, kuwekwa kwa taa kwenye barabara hizo ni
utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais aliyetaka miundombinu ya barabara
jijini Dodoma kuboreshwa, hali inayoongeza usalama kwa watumiaji wa
barabara hizo pamoja na kupandisha hadhi ya jiji na makazi ya maeneo
husika.
“Taa
hizi ni za kisasa na zitasaidia uhifadhi wa mazingira kwakuwa zinatumia
mwanga wa jua, Serikali inajitahidi kuboresha miundo mbinu ikiwemo
barabara hii, hivyo wananchi ambao barabara inapita katika makazi yao
hawanabudi kuilinda miundombinu ya taa hizi. Fedha za walipakodi
zimetumika hapa itasikitisha kuona miundo mbinu ya taa hizi kukuta
imeharibiwa” amesisitiza Kamuzora.
Awali,
akielezea shughuli zinazoendelea katika barabara ya Emmaus-African
Dream, Meneja wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) mkoani
Dodoma, Mhandisi Lusako Kilembe alibainisha kuwa taa hizo ni za kisasa
na zina uwezo wa kuhifadhi umeme hivyo zitasaidia kupunguza ghrama za
uendeshaji na uhakika katika matumizi ya barabara hizo.
Kampuni
ya Mionzi Jua Ltd ndiyo inayofanya kazi ya kuweka taa katika barabara
za Kisasa na Emmaus-African Dream, ambapo jumla ya kiasi cha Shilingi
milioni 287.1 zitatumika kukamilisha kazi hiyo.
IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA MAWASILINO SERIKALINI
OFISI YA WAZIRI MKUU
Mpekuzi.
Comments