Afariki baada kusukumwa ulevini.

MTU mmoja aliyefahamika kwa jina la Khalid Khamis Abdalla (60) mkaazi wa Kitumba amefariki dunia baada ya kusukumwa na Omar Mohammed Omar (18) mkaazi wa Kinuni.

Akizungumza na wandishi wa habari Kamishna Msaidizi wa Polis ambae ni Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Haji Khamis Haji, alisema tukio hilo limetokea Juni 30 ya mwaka huu huko Amani baa CCM.

Alisema marehemu huyo ambae anajulikana kwa jina la umaarufu Pinda, alikutwa na mauti akiwa ameshalewa na mwenzake alikuwa ameshalewa hivyo alimsukuma na kuanguka chini nakusababisha kutoka damu iliyomsababisha kupoteza maisha.

Sambamba na hayo, alifahamisha kwamba mtuhumiwa huyo anashikiliwa na Jeshi la Polisi, ili kuendelea na uchunguzi juu ya tukio hilo na utapokamilika atafikishwa Mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.

Akitaja matukio mengine Kamanda huyo alisema ndani ya wiki hiyo, wamepokea makosa manane ya unyanyasaji wa kijinsia.

Aliyataja makosa hayo kuwa ni kubaka yalikuwa matatu, kulawiti moja, kukashifu mawili na kutorosha mawili, ambapo katika makosa hayo watu wawili wanashikiliwa na Jeshi hilo kwa hatua zaidi za kisheria.

Sambamba na hayo alitumia fursa hiyo kuitaka jamii kushirikiana na Jeshi hilo, ili kuweza kuwakamata watu wengine wanaohusika.

Zanzibarleo.

Comments