ZEC yapiga mbiu ya mgambo Jang’ombe.

TUME ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), imetangaza rasmi tarehe ya uchaguzi mdogo wa jimbo la Jang’ombe, baada ya aliekuwa Mwakilishi wa jimbo hilo, Abdalla Diwani, kuvuliwa uanachama na CCM.
Taarifa hiyo ilitolewa jana na Mkurugenzi wa tume hiyo, Salum Kassim Ali.
Alisema uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Oktoba 27 mwaka huu, ambapo kazi ya uchukuaji fomu kwa wataowania nafasi hiyo, itaanza Oktoba 3 hadi 8 mwaka huu.
Alisema uwekaji wazi pingamizi na uteuzi wa wagombea unatarajia kuanza Oktoba 9, huku uteuzi wa wagombea utafanyika Okotoba 10 na kampeni zitaanza Oktoba 11 hadi 25.
Aidha alisema tume hiyo imemteuwa Mabruk Jabu Makame kuwa Makamu Mwenyekiti, ikiwa ni utekelezaji wa masharti ya kifungu cha 119 (2)(b) cha katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Tume hiyo imeviomba vyama vya siasa na wanachi wa jimbo la Jang’ombe kujitayarisha na uchaguzi huo.
Zanzibarleo.

Comments